Lebo

17/12/2014



ASOMAYE NA AFAHAMU {TUREJEE EDENI}

Chimbuko la Bamia ni Abyssinia (Ethiopia) Kisha ikaenea Duniani kote.

1. Michirizi na utonvu unaopatikana katika Bamia, husaidia kusawazisha Kisukari kwa kuzuia kiwango cha Sukari inayotumika katika mwili kutoka kwenye utumbo mkubwa.

2. Utelezi wa bamia huchuja uchafu unaoingia katika Kolestorali (cholesterol) na asidi ya Nyongo unaoingia kutoka kwenye Ini ambao usipo dhibitiwa huenda ikasababisha matatizo ya ki-afya.

3. Bamia husaidia kulainisha Utumbo mkubwa (large intestines) kutokana na kazi yake ya kulainisha choo.

4. Bamia hutumika kwa kutibu vidonda vya Tumbo inasaidia kusawazisha Asidi.
Magonjwa Maalum

5.Asidi ya Kujirudia rudia na Kufunga Choo
Tafuna vipande sita vya Bamia bila kutumia dawa nyigine kilasiku Asidi ya Kujirudia rudia na kufunga choo kutakwisha, inashusha Sukari kutoka 135 hadi 98

6.Pumu
Bamia ina Vitamin C ambayo inawafana watoto wanaougua ugonjwa wa pumu kupumua vizuri wanapoitumia. Nusu kikombe ya Bamia iliyopikwa huwa na miligramu 13 ya vitamin C.

7.Kidonda Ndugu (Cancer)
Bamia husaidia kuweka Utumbo kuwa na hali nzuri hivyo kupunguza uwezakano wakuugua ugonjwa huu wa Kansa hasa kwenye utumbo mkubwa.

8.Mishipa midogo ya Damu Kula Bamia kwa wingi kunasaidia kuimarisha Mishipa midogo ya Damu.

9.Cataracts{MTOTO WA JICHO}

Nusu kikombe cha Bamia iliyopikwa inakua na kiwango cha 460 IU ya vitamin A.ambayo inapunguza uwezakano wa kupata ugonjwa wa mtoto wa jicho (cataracts).

10.Usongo (Depression) na Kukosa Nguvu. Bamia ni mboga bora zaidi kwa wale wanaojisikia dhaifu, Kuchoka na wanao athirika na Usongo (depression).

10/12/2014

ASOMAYE NA AFAHAM



"Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi
kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi
akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi"
(Dan. 1:8). Ni ujasiri ulioje! Ombi lake halikuwa rahisi
kukubaliwa na msimamizi yule kwa vile angekatwa kichwa kama
wangeonekana wamekondeana (Dan. 1:10). Basi Danieli akamwambia,

"Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda wa siku kumi; na
watupe mtama [nafaka, kokwa, mboga za majani, matunda] tule, na
maji tunywe. Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za
wale vijana wanaokula chakula cha mfalme..." (Dan. 1:13).
Akawakubalia ombi hilo.

Je! mambo yalikuwaje kiafya baada ya
siku zile kumi tu? "Nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi [wanawake
wanaohangaika na vipodozi vinavyodhuru afya wangezingatia hilo],
na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote
waliokula chakula cha mfalme. Basi yule msimamizi akaiondoa
posho yao ya chakula [cha mfalme], na ile divai waliyopewa
wanywe, akawapa mtama [nafaka, kokwa, mboga za majani, matunda] tu" (Dan. 1:15,16).

Chakula cha matajiri au wafalme tunachokitamani sana
hakileti afya mwilini. Chakula rahisi cha mimea na maji safi na
salama ni lishe bora. Kwa akili safi na mwili wenye afya,
ulionenepa kiafya sio kwa ugonjwa, tumia vyakula vya mimea na
maji safi na salama, na kufuata Kanuni zile 8 za Afya. Wanasayansi wamegundua kuwa wale wanaokula vyakula vya mimea bilanyama wanaishi maisha marefu sana kuliko wanaokula nyama Danieli naye aliishi zaidi ya miaka 80 kufikia kipindi cha utawala wa Koreshi (Dan. 1:21; 10:1)

Hebu tuwafuatilie vijana wale wanne mwisho wa mafunzo yao ya miaka mitatu. Mfalme Nebukadreza aliwaonaje?
"Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote
hawakuonekana waliokuwa kama Danieli, na Hanania, na Mishaeli,
na Azaria... Na katika kila jambo la hekima na ufahamu
alilowauliza mfalme, akawaona kuwa wanafaa mara kumi zaidi ya
waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake" (Dan.1:19,20).

Kwa nini tuhangaike sana na suala la afya ya mwili wetu,
je! maisha ya kiroho si bora zaidi? "Mpenzi naomba ufanikiwe
katika mambo yote na kuwa na afya yako [kimwili], kama vile roho
yako ifanikiwavyo" (3 Yohana 2).

Wahenga walisema,

"Akilitimamu katika mwili wenye afya." Ni shauri la kuzingatiwa sana.
Kanuni ya Biblia ni hii: "

Basi, mlapo, mnywapo, au mtendapo
neno lo lote fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu" (1 Kor. 10:31).
Tunawajibika kuitunza miili yetu katika hali ya afya nzuri
kadiri iwezekanavyo (l Kor. 6:19,20; 1 Pet. 1:18,19;
Rum.12:1,2).

Suala la afya linahusu wokovu wetu. Mungu anaweza
kututumia kama Danieli (Dan. 1:17).

03/12/2014

Ndivyo ilivyo!!!

Ni kweli kabisa kwa WANAUME  halisia kwa hakuna manyanyaso,zarau wala haina yoyote ya kuwafanya au kuwa kuchukulia wanawake  kuwa hawana thamani