Basi mtiini Mungu.Mpingeni Shetani,naye atawakimbia Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi,na kuishafisha mioyo yenu,enyi wenye nia mbili{Yakobo 4:7-8} Submit yourselves then, to God, Resist the devil,and he will flee from you.come near to God and he will. come near you.wash your hands you sinners and purify your hearts you double minded.{James 4:7-8}NIV
02/02/2015
SIRI YA MTINDO WA MAISHA ULETAO AFYA
Watafiti wanaoishi katika kipindi hiki tulicho nacho wamejitahidi sana kuithibitisha ile kweli iliyothibitishwa kwanza na Biblia kwa kutoa maelezo haya:
Wanadamu ni viumbe kamili Mara nyingi kile tunachokigawa katika sehemu za kimwili, kiakili, na kiroho ni sehemu za mtu zilizo na uwiano unaoingiliana, wala hazitenganishiki kwa maneno mengine, kinachoidhuru akili, kinaudhuru mwili.
Hali yetu ya kiroho ina shinikizo lake juu ya hali yetu ya kimwili, na kinyume chake. Sisi ni watu kamili.
Kwa mfano watafiti wa kisayansi katika uchunguzi wao uliodhibitiwa wamegundua kwamba kicheko kile kitokanacho na furaha na shangwe huleta mabadiliko yanayoweza kupimwa katika mfumo wa kinga mwilini mwa mtu unaweza kabisa kuusaidia mwili wako kupigana na ugonjwa kwa vizuri zaidi ukiwa na furaha uchunguzi huo huonyesha jinsi akili na mwili vinavyofanya kazi yao kwa pamoja kwa ushirikiano wa karibu sana.
Katika maelfu ya miaka iliyopita Neno la Mungu lilidokeza kuwapo kwa uhusiano huo wenye nguvu kati ya akili na mwili ambao ni hivi karibuni tu umekubaliwa na kuingizwa katika nadharia ya kiganga:
"Moyo uliochangamka ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka huikausha mifupa" - (Mithali 17:22)
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)