Lebo

19/04/2015

JE, WAFU WANAWEZA KUONGEA NASI somo la 2?

Fundisho lisemalo kwamba mtu anapokufa anaendelea kuishi, hasa imani ile isemayo
kwamba roho za wafu zinarudi kuja kuwatumikia walio hai, limetayarisha njia kwa dini
ya siku hizi ya kuongea na mizimu (modern spiritualism).

Kama wafu wanaruhusiwa kufika mbele za Mungu na mbele ya malaika watakatifu, na kupewa uwezo wa kuwa na maarifa yanayozidi yale waliyokuwa nayo kwanza, kwa nini, basi, wasirudi duniani na kugawa maarifa yao na kuwafundisha walio hai? Iwapo roho za wafu zinarukaruka juu ya
[vichwa vya] rafiki zao waliomo duniani humu, kama wafundishavyo wanatheolojia hao
wanaopendwa sana na watu wengi,

EBU jiulize kwa nini, basi, wasiruhusiwe kuongea nao, na kuwaonya dhidi ya maovu, ama kuwafariji katika huzuni zao?



Ni kwa jinsi gani wale wanaoamini kwamba mtu akifa roho yake inaendelea kuishi wanaweza KUIKATAA nuru ile inayowajia kama nuru itokayo mbinguni ambayo inaletwa na pepo [roho] hao
wenye utukufu?

Hapo ndipo ipo njia inayodhaniwa kuwa ni takatifu, ambayo Shetani anaitumia kutekeleza MAKUSUDI yake. Malaika wale walioanguka ambao wanatekeleza amri zake [Shetani] wanakuja kama wajumbe wanaotoka katika ulimwengu wa roho. Wakati [wenye dini ya mizimu] wanadai kwamba wanawaleta walio hai katika mawasiliano na wafu, hapo ndipo yule mkuu wa uovu anapotumia nguvu yake ya uchawi juu ya mioyo [akili] yao [hao walio hai].

JE, WAFU WANAWEZA KUONGEA NASI?


Huduma ya malaika watakatifu, kama ilivyoelezwa katika Maandiko, ni ukweli wenye
faraja kuu na wa thamani kwa kila mfuasi wa Kristo.Walakini fundisho la Biblia juu ya jambo hili limetiwa giza na kupotoshwa kwa njia ya makosa yanayotokana na theolojia inayopendwa sana na watu wengi.

Fundisho lile lisemalo kwamba mwanadamu ana roho isiyokufa, ambalo liliazimwa kwanza kutoka kwa falsafa ya kipagani, na hatimaye wakati wa giza lile la UASI MKUU likaingizwa katika imani ya Kikristo, limechukua mahali pa ile kweli, inayofundishwa kwa wazi kabisa katika Maandiko, kwamba

 "WAFU HAWAJUI NENO LO LOTE." Watu wengi sana wamekuja kuamini kwamba ni roho za
wale waliokufa "watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu."
Walakini [imani] hiyo ni kinyume na ushuhuda wa Maandiko yanayohusu kuwako kwa
malaika mbinguni, na uhusiano wao na historia ya mwanadamu, kabla ya [kutokea] kifo
cha mwanadamu ye yote.