Basi mtiini Mungu.Mpingeni Shetani,naye atawakimbia Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi,na kuishafisha mioyo yenu,enyi wenye nia mbili{Yakobo 4:7-8} Submit yourselves then, to God, Resist the devil,and he will flee from you.come near to God and he will. come near you.wash your hands you sinners and purify your hearts you double minded.{James 4:7-8}NIV
22/09/2016
Kukua Katika Kristo
KULE kuongoka moyo ambako kunatufanya tupate kuwa watoto wa Mungu, kumenenwa katika Biblia kama ni kuzaliwa. Tena kumelinganishwa na kuota kwa mbegu njema zilizopandwa na mkulima. Vivyo hivyo wale ambao wameongoka moyo na kuanza kumfuata Kristo ni kama “watoto wachanga,” (1 Petro 2:2), tena lazima wakue hata wawe kama watu wazima katika Kristo Yesu. Au kama mbegu njema zilizopandwa shambani zinavyokua, nao wanapaswa kukua na kutoa matunda mema ya kiroho.
Isaya asema hivi juu yao, “Wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe.”
Isa. 61:3. Hivyo kutoka katika viumbe vya asili hutolewa vielelezo ili vipate kutusaidia sisi kuzielewa vizuri zaidi zile kweli za ajabu za maisha ya kiroho. Akili zote na ustadi wote wa mwanadamu haviwezi kamwe kukipa uhai kitu chochote kilicho kidogo sana katika maumbile.
Ni kwa uhai ule tu alioutoa Mungu mwenyewe mmea au mnyama anaweza kuishi. Hivyo ni kwa njia tu ya uhai utokao kwa Mungu maisha ya kiroho hupatikana ndani ya mioyo ya wanadamu. Mtu “asipozaliwa mara ya pili” hawezi kushiriki uzima ule ambao Kristo alikuja kutupa sisi. Yoh. 3:3,5.
Kama ilivyo katika kupata uzima, ndivyo ilivyo katika kuendelea kukua. Ni Mungu anayelifanya chipukizi lichanue na ua ligeuke na kuwa tunda. Ni kwa uwezo wake mbegu inakua, “kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke.” Marko 4:28.
Naye Hosea nabii anasema kuhusu Israeli ya kwamba “atachanua maua kama nyinyoro.” “Watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu.” Hosea 14:5,7. Na Yesu anatuagiza anasema, “Yatafakarini maua jinsi yameavyo.” Luka 12:27. Mimea na maua havikui kwa kujitunza na kuhangaika na kujitahidi vyenyewe, bali kwa kuvipokea vile anavyotoa Mungu ili kuendesha uzima wao. Mtoto, kwa kuhangaika kwake au kwa nguvu zake mwenyewe, hawezi kuongeza urefu wake. Na wewe pia, kwa kuhangaika kwako na juhudi zako mwenyewe, huwezi kuendelea kukua katika mambo ya kiroho. Mmea au mtoto hukua katika mazingira yake kwa kupokea vile vinavyoweza kusaidia kuendesha uzima wake,hewa, mwanga wa jua, na chakula. Jinsi vitu hivyo
vya asili vinavyofaa kwa uhai wa mnyama na mmea, ndivyo Kristo alivyo kwa wale wanaomtumaini. Yeye kwao ndiye “nuru ya milele,” “ni jua na ngao.” Isa. 60:19; Zab. 84:11. Atakuwa “kama umande kwa Israeli.” “Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa.” Hosea 14:5; Zab. 72:6. Yeye ndiye maji ya uzima, “mkate wa Mungu ushukao kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.” Yoh. 4:14; 6:33,35.Katika ile zawadi ya Mwanawe isiyo na kifani, Mungu aliizungushia dunia yote hewa ya neema yake ambayo ni halisi kama hewa inayoizunguka dunia.
Wale wote wanaochagua kuvuta hewa hii iletayo uzima wataishi, na kukua hadi kufikia kimo cha
wanaume na wanawake katika Kristo Yesu. Kama ua linavyolielekea jua, ili mionzi inayong’aa iweze kusaidia katika kuukamilisha uzuri wake na umbile lake linganifu, ndivyo itupasavyo sisi kuligeukia Jua la Haki, ili nuru ya Mbinguni ipate kung’aa juu yetu, ili tabia yetu iweze kukua na
kufanana na ile ya Kristo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)