A Call to the Youth _ PART 10
Make it the law of your life from which no temptation or side interest shall cause you to turn,Through Jesus Christ show that you are worthy of the sacred trust with which the Lord has honored you in bestowing upon you life and grace. You are to refuse to be in subjection to the power of evil. As soldiers of Christ we must deliberately and intelligently accept His terms of salvation under every circumstance, cherish right principles, and act upon them. Divine wisdom is to be a lamp to
your feet. Be true to yourselves, be true to your God.
Everything that can be shaken will be shaken; but rooted and grounded in the truth, you will abide with those things that cannot be shaken. The law of God is steadfast, unalterable; for it is the expression of the character of Jehovah. Make up your mind that you will not by word or influence cast the least dishonor upon its authority.
Basi mtiini Mungu.Mpingeni Shetani,naye atawakimbia Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi,na kuishafisha mioyo yenu,enyi wenye nia mbili{Yakobo 4:7-8} Submit yourselves then, to God, Resist the devil,and he will flee from you.come near to God and he will. come near you.wash your hands you sinners and purify your hearts you double minded.{James 4:7-8}NIV
10/08/2015
KUTUBU - 5
TUMEWEZA KUONA Sala ya Daudi baada ya kuanguka kwake dhambini inatudhihirishia vizuri
jinsi huzuni ya kweli kwa ajili ya dhambi ilivyo hasa. Kutubu kwake
kulikuwa kwa kweli na kwenye kina. Kutubu kwa namna hii hakuwezekani kwetu sisi kwa uwezo wetu wenyewe;
kunawezekana katika Kristo tu, aliyepaa juu na kuwapa wanadamu vipawa.
Hapo ndipo wengi wanapopotea, na hivyo hushindwa kupokea msaada anaotaka kuwapa Kristo. Wao wanadhani kwamba hawawezi kuja kwa Kristo isipokuwa kwanza wawe wamekwisha kutubia
dhambi zao, na ya kwamba kutubu kunawaandaa kupokea msamaha kwa ajili ya dhambi zao. Ni kweli kwamba kutubu kunakuja kabla ya msamaha wa dhambi; maana ni moyo ule tu uliovunjika na kupondeka, unaoona kwamba unamhitaji Mwokozi. Lakini je! ni lazima mwenye dhambi angoje mpaka amekwisha tubu kabla ya kwenda kwa Yesu? Je! toba iwe kizuizi kati ya mwenye dhambi na Mwokozi?
Katika Biblia, yaani, Neno la Mungu, hatusomi kwamba mwenye dhambi hana budi kutubu kabla ya kukubali mwito wa Kristo asemaye, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” Mt. 11:28. Ni uwezo unaotoka kwa Kristo unaowawezesha watu kutubu kweli kweli. Petro aliwaeleza Waisraeli mambo haya kwa dhahiri aliposema, “Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.” Mdo. 5:31.
Kadiri tusivyoweza kusamehewa dhambi bila Kristo, ndivyo tusivyoweza kutubu pasipo Roho wa Kristo kuziamsha dhamiri zetu. Kristo ndiye asili ya kila fikara njema. Yeye tu ndiye awezaye kupanda mbegu ya kuchukia dhambi katika moyo. Kila tamaa moyoni mwetu ya kutaka kuijua kweli na kuwa na maisha safi, kila kusadikishwa moyoni mwetu kunakotuonyesha kuwa sisi ni wenye dhambi, ni ushahidi uonyeshao kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi mioyoni mwetu.

Waliopewa Kitabu - 2
Aya hizi ni NUKUU kutoka DivineIslam’s Qur’an Viewer software v2.913
Kurani Tukufu yasema hivi kuhusu kundi hilo la pekee, kwamba hao “ndio miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli”. Iwapo hao ni miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli, basi yale wayasadikiyo hayana budi kuwa ndiyo kweli yenyewe. Kama Mwenyezi Mungu anawaita kuwa wamo miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli, basi, sisi hatuthubutu kabisa kuwakosoa.
Lakini je! si afadhali sisi pia tungeweza kujifunza kitu kwao?
Twaona ya kwamba watu hao wa pekee wanakishikilia kile ‘Kitabu’ (Maandiko ya Biblia) ambacho
Nabii Muhammad kwa makusudi mazima alituelekeza sisi kwenye [Kitabu] hicho katika Kurani Tukufu (Al Maidah) Sura 5:46 … “Na tukawafundisha (Mitume hiyo) Isa bin Maryamu
kuyahakikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uongozi na nuru na isadikishayo yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na uongozi na mauidha kwa wamchao (Mwenyezi Mungu).”
Watu hao wanasadiki kwamba ni jukumu lao kujitoa kabisa kwa Mwenyezi Mungu pasipo kuzuia kitu, kuwa na utii kwake usio na swali. Watu hao wana maadili ya kiwango cha juu, ambayo yamejengwa juu ya Maandiko ya Biblia.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)