Lebo

14/07/2015

Jinsi Mungu Anavyompenda Mwanadamu- 2


Ingawa dunia imeanguka katika hali mbaya kwa ajili ya dhambi, lakini yote yaliyomo si huzuni na mashaka. Viumbe vya ulimwengu vimekuwa kama mitume waMungu kutuletea habari za faraja na utulivu. Kila mti wa miiba una maua yake pia; yaani, katika kila shida twaweza kupata baraka za Mungu.

“Mungu ni pendo” imeandikwa juu ya kila chipukizi, juu ya ncha ya kila jani dogo linalochipua. Ndege wazuri wanaoijaza anga na nyimbo zao za furaha, kila aina ya ua lililotiwa rangi nzuri katika ukamilifu wake likitia harufu yake nzuri katika hewa, miti mirefu sana ya msituni pamoja na majani yake mazuri ya kijani kilichokolea yote hutushuhudia upendo na utunzaji wa Mungu, jinsi anavyotaka kuwafurahisha watoto wake.