Na hatimaye gari hii ndiyo iliyo chaguliwa liweze kutumika katika safari ya kuwatoa wanaKIU kuanzia chuoni hapa mpaka uko NIT kwa lengo kushiriki FIDERATION iliyo mbele yao.
Kama MUNGU wetu aishivyo vijana walianza safari kwa OMBI maalum toka kwa MWENYEKITI na kupitia uhuduma hii waliweza kusafiri salama hatimaye walisali salama
Ni jambo la kumshukuru MUNGU tuliweza kufika mapema na kuwahi sehemu fupi ya shule ya sabato na baada ya kumaliza shule ya sabato lilifuata SOMO MAALUMU toka kwa muinjilisti Christopher Mang`ombe na somo lake lilisema ALAMA YA UTAMBULISHO.
Vijana nao walikuwa makini sana kusikiliza mafundisho toka kwa muinjilisti kama umekosa kufika hapa ebu jitaidi sasa katika programu za mchana uwe pamoja nasi.
Vijana wa KIU pia waliweza kupata nafasi ya kuhudumu kwa njia ya uimbaji.
Kwa habari na matukio ya mchana yaliyo endelea hapa karibu sana na usisite kutembelea na kualika wenzako pia nawe utabarikiwa sana.