Lebo

14/02/2015

BAADHI YA MATUKIO KATIKA FIDERATION ILIYOFANYIKA CHUO CHA USAFIRISHAJI(NIT)


Ilikuwa  ni  asubuhi  ya  kipekee sana  kwa maana  ni siku  ambayo  ilikuwa ikisubiriwa  kwa  hamu  sana  na  wengii wetu  kwa  kuthibitisha  hili  vijana  wa  KAMPALA  walifika  mapema  sana  katika  eneo  la  maegesho  ilikujua  ni  namna  gani  wataweza  kuwa  katika  eneo  la tukio.


Na  hatimaye  gari  hii ndiyo  iliyo chaguliwa liweze kutumika  katika  safari  ya  kuwatoa  wanaKIU kuanzia  chuoni  hapa  mpaka  uko  NIT kwa  lengo  kushiriki  FIDERATION iliyo  mbele  yao.


Kama   MUNGU  wetu  aishivyo  vijana  walianza  safari  kwa OMBI  maalum toka  kwa  MWENYEKITI na kupitia  uhuduma  hii waliweza  kusafiri salama  hatimaye walisali salama



Ni jambo   la  kumshukuru  MUNGU   tuliweza  kufika  mapema  na kuwahi  sehemu  fupi  ya  shule  ya  sabato na  baada  ya  kumaliza  shule  ya  sabato  lilifuata  SOMO MAALUMU  toka  kwa  muinjilisti  Christopher Mang`ombe na  somo  lake  lilisema ALAMA  YA  UTAMBULISHO.



Vijana  nao  walikuwa  makini  sana  kusikiliza  mafundisho  toka  kwa  muinjilisti kama  umekosa  kufika  hapa  ebu  jitaidi  sasa  katika  programu  za  mchana  uwe pamoja  nasi.


Vijana  wa   KIU  pia  waliweza  kupata  nafasi  ya  kuhudumu  kwa  njia  ya  uimbaji.



Kwa   habari  na matukio  ya  mchana  yaliyo  endelea  hapa  karibu  sana  na  usisite  kutembelea na  kualika  wenzako  pia  nawe  utabarikiwa  sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Tuandikie maoni yako hapa. Leave your comments here