Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani Dr Ted
Wilson amewasili Juba,Sudan ya Kusini akitokea nchini Tanzania baada ya
kushiriki kwenye sherehe za utume wa kanisa hilo(Mission Extravaganza)
zilizofanyika kwa juma zima toka februari mosi mwaka huu na kuhitimishwa kwenye
uwanja wa Taifa kuanzia Februari 4 hadi 7,mwaka huu.
Ted akiwa nchini Tanzania
aliongoza ibada ya siku ya Sabato ambapo alihutubia waumini wa kanisa hilo
wapatao 50,000 wanaounda Divisheni ya Afrika
Mashariki na Kati yenye nchi 11,huku ukihudhuriwa na Makamu wa Rais Dr Mohamed
Gharib Bilal ambaye alizindua mkutano huo akiwataka waumini hao kuombea taifa
la Tanzania kudumisha amani,upendo na mshikamano.
Mkutano huo ambao pia
ulihudhuriwa na viongozi wandamizi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato toka
yalipo makao makuu yake huko Washngton DC,Marekani ulishuhudia Waziri wa Mambo
ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe akiufunga kwa kulipongeza na
kulitaka kanisa hilo kutojiingiza katika migogoro ya aina yoyote. Ted Wilson akiwa
ameambatana na viongozi wengine wa Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati
aliwasili Juba na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo nchini humo
ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kutembelea nchini hiyo toka
ilipojitenga na Sudani julai 9,2011.