Lebo

17/01/2015

“MSIRUKE MIPAKA KWA KUVUNJA TAADHIMA YA SABATO (JUMAMOSI) ”

Tuangalie leo QURAAN tukufuu inatuambia NINI?

BISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

Leo kuna somo jingine zuri sana la kujifunza.

Je,kwa Waislamu na watu wengine wanapaswa kuitunza siku ya Sabato “Sabt” kama siku ya kupumzika ambayo mtu hujizuia asifanye
kazi yoyote?

Wengi katika dini ya Kiislamu huamini kwamba zile Amri
Kumi zilizoandikwa kwa “kidole chake Mwenyezi Mungu”
(Allah) hazina budi kutiiwa. Kile ambacho wengi
wamepitiwa ni ukweli kwamba moja wapo ya hizi “Amri
Kumi” imesahauliwa.

Hata Wakristo wengi wanaodai kukifuata Kitabu hicho (Vitabu Vitakatifu vya Biblia) hawaijali moja ya hizo Amri kama zilivyoandikwa katika Taurati. Kusema kweli wengi wao wanaziangalia kwa chuki kubwa au kwa dharau kubwa Sheria hizo ambazo ni Takatifu kwa wanadamu.

Kwanza, twataka kujadili hoja hii, Je, Amri Kumi ni nini?

Je, hivi yatupasa sisi kuishi kwa kuzifuata sheria hizi siku hizi?

Twataka kuziangalia kwa makini hizo Amri Kumi kuona ni nini hasa. Zimeandikwa katika Taurati katika Kutoka 20 na Kumbukumbu la Torati 5 la (Vitabu Vitakatifu) na katika Injili yote ya Maandiko ya Biblia.

Mkumbukeni Mstahiki Nabii Muhammad kile alichokifunua katika Kurani Tukufu kwamba Taurati iliyoteremshwa kwa Musa na Injili aliyopewa Isa al-Masih, vyote viwili vilikuwa kwa ajili ya mauidha kwetu. Hivyo kwetu ni uongozi, nuru, na kipimo cha hukumu.

Angalia:
Sura 2:53 Al Baqarah
Sura 3:3 Aali Imran
Sura 21:48 Al-Aniva
Sura 10:94 Yunus
Sura 5:44 Al Maidah

Sura hizi ni baadhi tu ya kumbukumbu nyingi zilizomo ndani ya Kurani Tukufu kuhusu hivyo Vitabu Vitakatifu vya Maandiko ya Biblia (Taurati na Injili).Kielelezo cha Ibrahimu…

Watu wengi leo huona kwamba Ibrahimu yule wa zamani, alikuwa ni mtu aliyemheshimu Mwenyezi Mungu kwa moyo wake wote. Hivyo yeye amekuwa kielelezo fulani kwetu cha kufuata. Katika Vitabu vile Vitakatifu (Maandiko ya Biblia) twaambiwa yafuatayo kuhusu
Ibrahimu na jinsi alivyoziona zile Amri Kumi za Mwenyezi
Mungu.

Katika Taurati, Mwanzo 26:5 “… Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.”

Aya hii katika Taurati hutuambia sisi kwamba Amri Kumi za Mwenyezi
Mungu zilifuatwa na Ibrahimu aliyeishi muda mrefu kabla ya siku za Musa. Hiyo pia inatuambia sisi ya kwamba watu wa nyakati zile za kale waliijua fika sheria ile ile ambayo pia ilirudiwa kwa Musa katika vilele vile virefu vya Mlima Sinai. Iwapo Ibrahimu anafikiriwa kuwa ni “Hanif” kati ya wale ambao kwa unyofu wa moyo wanamkaribia sana

Mwenyezi Mungu, basi, sisi tungefanya vema kukifuata
kielelezo chake Ibrahimu kwa kuzitunza pia Amri Kumi za
Mwenyezi Mungu. Kufanya mambo yawe rahisi, hii
maana yake ni kwamba Ibrahimu aliitunza Siku ya Saba ya
juma kama siku ya ‘kupumzika’ kwa heshima yake
Mwenyezi Mungu


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Tuandikie maoni yako hapa. Leave your comments here