Lebo

20/04/2015

JE, WAFU WANAWEZA KUONGEA NASI somo la 3?

Shetani anao uwezo wa kuleta mbele ya wanadamu mfano [kivuli] wa ndugu zao waliokufa. Mfano huo [umbile la marehemu] unakuwa kamili; mtazamo wake huwa ni ule ule waliouzoea kuuona, maneno yake, sauti yake, huigwa kabisa kwa namna ya kushangaza sana.

Wengi hufarijika kwa matumaini ya kwamba ndugu zao wapendwa wanafurahia raha isiyo na kifani kule mbinguni, na bila kushuku hatari inayowakabili, wanatega sikio lao "wakisikiliza roho [mapepo] zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani." [l Timotheo 4:l.]

Baada ya kusadiki kwamba wafu wanarudi kweli na kuongea nao, Shetani anafanya watokee wale walioingia makaburini mwao wakiwa hawajajiweka tayari [yaani, waovu].Hao hudai kwamba wanayo furaha mbinguni na ya kwamba wanakalia hata vyeo vya juu kule, na kwa njia hiyo uongo unaenezwa kote kwamba hakuna tofauti yo yote kati ya
wenye haki na waovu.


Wageni hao wasemao uongo [mapepo] wanaowatembelea [wanadamu] kutoka katika ulimwengu wa roho wakati mwingine wanatoa tahadhari na maonyo ambayo hutokea kuwa ni ya kweli. Basi, imani [ya walio hai] inapoimarishwa hivyo, wanaanza kutoa mafundisho ambayo moja kwa moja yanaihafifisha imani [ya watu hao] katika Maandiko.

Huku wakijionyesha kuwa wanapenda sana kuwaona marafiki zao waliomo duniani wakiwa na hali njema ya maisha, wanapenyeza mafundisho ya uongo kwa hila ambayo ni ya hatari sana [kiroho]. Ukweli wa kwamba wanatoa baadhi ya mafundisho yaliyo ya kweli, na wakati fulani wanaweza kubashiri matukio yatakayotokea baadaye, hufanya maneno yao wanayosema yawe na mwonekano
wa kutegemewa; mafundisho yao ya uongo yanapokelewa kwa upesi na watu wengi sana, na kusadikiwa kabisa [pasipo shaka lo lote], kana kwamba [maneno hayo] yalikuwa ni zile kweli takatifu sana za Biblia.


Sheria ya Mungu [Amri Kumi] huwekwa kando, Roho wa neema anadharauliwa, na damu ile ya agano inahesabiwa kuwa ni kitu kilicho najisi. Roho hizo [mapepo] zinakana Uungu wa Kristo na hata zinamweka Muumbaji kuwa yuko sawa nazo. Hivyo chini ya umbo hilo jipya la kuigiza Mwasi yule Mkuu [Shetani] bado anaendelea na pambano lake dhidi ya Mungu lililoanza kule mbinguni na
[sasa] ni karibu miaka elfu sita limeendelezwa duniani humu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Tuandikie maoni yako hapa. Leave your comments here