Lebo

20/07/2015

KUTUBU


Sehemu ya 1

Je, mwanadamu anawezaje kuwa mwenye haki mbele za Mungu? Mwenye dhambi anawezaje kufanywa kuwa mwenye haki? Ni kwa njia pekee ya Kristo sisi tunaweza kupatanishwa na Mungu na kuwekwa katika hali ya utakatifu; lakini, je, twawezaje kufika kwake Kristo? Wengi wangali wakijiuliza swali lile lile kama walivyojiuliza watu wengi siku ile ya Pentekoste walipochomwa mioyo yao kwa ajili ya dhambi zao, na kulia, “Tutendeje?”


Neno la kwanza la jibu la Petro lilikuwa ni hili “Tubuni.” Mahali pengine pia alisema hivi, “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.” Matendo 2:38; 3:19. Kutubu kunajumuisha huzuni kwa ajili ya dhambi, na kugeuka kwenda mbali nayo. Hatutaikataa dhambi mpaka hapo tutakapoona ubaya wake ulivyo hasa; yaani, hapatakuwa na badiliko la kweli katika maisha yetu mpaka hapo tutakapogeuka katika mioyo yetu na kwenda mbali nayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Tuandikie maoni yako hapa. Leave your comments here