Basi mtiini Mungu.Mpingeni Shetani,naye atawakimbia Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi,na kuishafisha mioyo yenu,enyi wenye nia mbili{Yakobo 4:7-8} Submit yourselves then, to God, Resist the devil,and he will flee from you.come near to God and he will. come near you.wash your hands you sinners and purify your hearts you double minded.{James 4:7-8}NIV
12/06/2016
Dalili za Kuwa Mwanafunzi wa Kristo........
HATA imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! yamekuwa mapya.” 2 Kor. 5:17. Pengine mtu hawezi kutaja siku wala mahali hasa alipoongoka kuwa mfuasi wa Kristo; lakini kukosa kufanya hivyo si kama kusema kwamba yule hakuongoka kweli. Kristo alimwambia Nikodemo, “Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.” Yoh. 3:8.Upepo hauwezi kuonekana, lakini twasikia na kuona matendo yake; na vilevile Roho wa Mungu anajulikana kwa namna ya matendo yake mioyoni mwa wanadamu.
Uwezo wake, usioonekana na macho ya kibinadamu, huanzisha maisha mapya moyoni; humwumba kuwa mpya kwa mfano wa Mungu. Ijapokuwa kazi ya Roho ni ya kimya kimya na haionekani kwa macho, matokeo yake huonekana waziwazi. Kama Roho Mtakatifu ameutengeneza moyo wa mtu kuwa mpya, jambo hilo litaonekana katika maisha yake. Ingawa sisi wenyewe hatuwezi kufanya lolote katika kuigeuza mioyo yetu, wala kujiweka wenyewe katika hali ya kupatana na Mungu; ingawa haifai kabisa kujitegemea wenyewe au matendo yetu yaliyo mema; maisha yetu yatadhihirisha kama tunayo neema ya Mungu mioyoni mwetu,Badiliko litaonekana katika tabia zetu, mazoea yetu, na shughuli zetu tunazozifanya.
Tofauti dhahiri na thabiti itaonekana kati ya maisha yetu yalivyokuwa zamani na vile yalivyo sasa. Tabia ya mtu fulani hujulikana si kwa matendo mema au mabaya ya siku moja moja tu, ila kwa mwelekeo wa matendo yake na maneno yake, na mazoea yake ya siku zote. Kweli yawezekana kwamba kuna watu ambao mienendo yao ni myema machoni pa wenzao, bila kuongoka moyo kwa njia ya Kristo. Kupenda kusifiwa na kuwa viongozi kati ya wengine, kwaweza kuwafanya waonekane kuwa ni wenye adabu. Kujistahi nafsi zetu kunaweza kutufanya tuyaepuke matendo mabaya ya nje. Moyo wenye uchoyo waweza kutenda matendo ya ukarimu. Ikiwa ni hivyo, twawezaje kuyakinisha kama tumekuwa upande wa Kristo, au sivyo? Ni nani anayeutawala moyo? Fikara zetu ni juu ya nani? Tumezoea kuongea juu ya nani? Ni nani ambaye tunampenda kuliko wote na kumtumikia kwa nguvu zetu zote?
Kama sisi tu watu wa Kristo, basi, fikara zetu zi pamoja naye, na fikara zetu tamu sana zi juu yake. Tunajitoa kwake pamoja na vyote tulivyo navyo. Twatamani kufanana naye, kuwa na Roho wake mioyoni, kufanya mapenzi yake na kumpendeza katika mambo yote. Wale wanaokuwa viumbe vipya katika Kristo Yesu watazaa matunda ya Roho, yaani, “upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.” Gal. 5;22,23. Hawatafuata tena tamaa zao za zamani, bali watamwamini Mwana wa Mungu na kufuata nyayo zake; tabia yake itaonekana katika maisha yao, nao watajitakasa kama yeye alivyo mtakatifu. Mambo waliyochukizwa nayo zamani, sasa watayapenda; na vile walivyovipenda zamani, sasa watachukizwa navyo. Wenye kiburi na wenye kujidai watageuka na kuwa wapole na wanyenyekevu. Watu wa ovyo na wale wanaojivuna watakuwa watu wa maana na wasio kimbelembele. Walevi wataacha ulevi wao, na waasherati na wazinzi watageuka na kuwa na maisha yaliyo safi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Tuandikie maoni yako hapa. Leave your comments here