Lebo

29/11/2014

ASOMAYE NA AFAHAMU

                    
Pombe haikuwa sehemu ya kinywaji ambacho Mungu alimpa
mwanadamu; maji safi na salama ndicho kinywaji bora kuliko
vyote kwa mwanadamu (Mithali 20:1; 23:29-35). Walevi
hawataurithi ufalme wa Mungu (1 Kor. 6:9,10; Gal. 5:21). Kuna
wengi wanaosema, "Mimi nakunywa sana, lakini silewi." Tatizo
la pombe sio kulewa tu, bali ni zile athari zinazotokana na
kunywa pombe ambayo ina sumu mbaya ya alkoholi. Sumu hiyo
huathiri vibaya moyo, mishipa ya fahamu, nyama za mwili na
kadhalika. Mungu atamharibu mtu ye yote anayeuharibu mwili wake
kwa makusudi kwa njia yo yote ile ----- pombe, tumbako, madawa
ya kulevya, na kadhalika (1 Kor. 3:16,17). Pia kuna vinywaji
vinavyopendwa na watu wengi aina ya 'Cola', Kahawa, na Majani ya
Chai ambavyo huidhuru mishipa ya fahamu, ubongo na mwili.
Viepukwe.

Bible says


27/11/2014

Ina aminika kuwa binadamu walitokana na mabadiliko ya viumbe fulani hii ni kwa mujibu wa sayansi na elimu zingine zinazotokana na uchunguzi wa kibinadamu madai haya si ya kweli hata kidogo na hakika yana pingana na elimu ya mafundisho katika vitabu VITAKATIFU

HAPO MWANZO

Hapo mwanzo  ulimwengu huu ulikuwa ukiwa na roho ya MUNGU ilikuwa juu  ya vilindi vya maji ndipo BWANA akaamua kuufanya upya ulimwengu huu katika kazi yake aliyofanya  ulimwengu huu uliwekwa  katika madhari  nzuri na hali ya kupendeza sana katika kazi yake ya juma zima aliweza kufanya viumbe watakaoishi katika ulimwengu huu wenye madhari nzuri ya yakipee  ebu twende pamoja tuone ni mambo gani na hali gani iliyoleta maaafa hapo baadae

Ujumbe wetu kwa ULIMWENGU!!!!