Lebo

08/08/2015

KUTUBU - 4


Sala ya Daudi baada ya kuanguka kwake dhambini inatudhihirishia vizuri jinsi huzuni ya kweli kwa ajili ya dhambi ilivyo hasa. Kutubu kwake kulikuwa kwa kweli na kwenye kina. Hapakuwa na
jitihada yo yote ya kupunguza ukubwa wa makosa yake; hakuwa na tamaa yo yote ya kuikwepa hukumu iliyotishiwa juu yake ambayo iliivuvia sala yake. Daudi aliuona ukubwa upitao kiasi wa kosa lake; aliona unajisi wa moyo wake; aliichukia sana dhambi yake. Hakuomba ili apate msamaha tu, aliomba pia ili awe na moyo safi. Alitamani sana kuwa na furaha iletwayo na utakatifu - yaani,
kurejeshwa katika hali ya amani na ushirika na Mungu. Hii ilikuwa ndiyo lugha ya roho
yake:


Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake.  Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila.” Zaburi 32:1-2. “Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu. Na dhambi yangu i mbele yangu daima Unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu. Usinitenge na uso wako, Wala Roho wako Mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi, Ee Mungu, Mungu wa wokovu wangu, Utuponye na damu za watu Na ulimi wangu utaiimba haki yako.” Zaburi 51:1-14. Kutubu kwa namna hii hakuwezekani kwetu sisi kwa uwezo wetu wenyewe; kunawezekana katika Kristo tu, aliyepaa juu na kuwapa wanadamu vipawa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Tuandikie maoni yako hapa. Leave your comments here