Lebo

08/08/2015

Waliopewa Kitabu - 1

Aya hizi ni NUKUU  kutoka DivineIslam’s Qur’an Viewer software v2.913


Assalamu’ alaikum! Kurani Tukufu huelekeza kidole chake kwenye kundi lile liitwalo “Waliopewa Kitabu”. Msomaji anaombwa asome Sura 3:113-115. Aali Imran. 003:113 “Wao (Waliopewa Kitabu) si wote sawa. Katika (hao) Waliopewa Kitabu wamo watu waliotengenea  wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu (yaani wamesilimu).” 003:114 “Wanamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanayaendea mbio mambo mema.

Na hao ndio miongoni mwa hao watendao mema (kweli kweli).” 003:115 “Na heri yo yote watakayoifanya hawatakanushiwa (thawabu zake). Na Mwenyezi Mungu anawajua wanaomcha (wakajiepusha na makatazo yake na wakafanya maamrisho yake).” 


 Watu hao wanajulikana kama ‘Wakristo’. Hao wanaitwa ‘Waliopewa Kitabu’ (Maandiko ya Biblia). Lakini miongoni mwao limo kundi la pekee. Kurani Tukufu yasema kwamba ipo tofauti kati ya hao ‘Wakristo’ na ya kwamba ‘si wote sawa.’

Je, kundi hilo la pekee ni akina nani ambao Nabii Muhammad (jina lake na liheshimiwe) alivuta mawazo ya watu kuelekea kwao kwa namna ya ajabu kama hiyo, ya kuwa wao ni ‘miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli’! Hebu zingatia tabia zinazolitambulisha kundi hili la pekee kutoka katika Sura 3:113-115
 

1. si (Wakristo) wote sawa
 

2. katika (hao) waliopewa Kitabu wamo watu waliotengenea
 

3. wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu
 

4. wanasujudu
 

5. wanamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho
 

6. wanaamrisha mema [wanafundisha kwa mamlaka yaliyo ya haki]
 

7. wanakataza maovu
 

8. wanayaendea mbio mambo mema [wanajitahidi kufanya yale yenye sifa njema]
 

9. hao ndio miongoni mwa hao watendao mema kweli
kweli
 

10. na heri yo yote watakayoifanya hawatakanushiwa. [Mwenyezi Mungu anawajua]

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Tuandikie maoni yako hapa. Leave your comments here