Aya hizi ni NUKUU kutoka DivineIslam’s Qur’an Viewer software v2.913
Nukuu ili ishia hapa )
Watu hao wanasadiki kwamba ni jukumu lao kujitoa kabisa kwa Mwenyezi Mungu pasipo kuzuia kitu, kuwa na utii kwake usio na swali. Watu hao wana maadili ya kiwango cha juu, ambayo yamejengwa juu ya Maandiko ya Biblia.ENDELEA HAPA
Wanamheshimu Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mkuu kuliko wote, tena hawana mshirika ye yote (kama vile Maryamu au wale wengine waitwao watakatifu wanaoabudiwa) ambaye wanamfungamanisha na huyo Mungu kama Wakristo wengi sana wafanyavyo. Katika Injili maneno haya hunenwa: Yakobo 2:19 “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema na katika Marko (Isa al-Masih) Kristo Mwenyewe alisema… “Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja”. Watu hao hawazisujudu sanamu katika ibada yao kama wafanyavyo Wakristo wengi sana.Wanasadiki kwamba kuabudu sanamu au mifano iwayo yote kumekatazwa kabisa na Mwenyezi Mungu, kama ilivyoandikwa katika Taurati, Kutoka 20:4-5 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala
mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia”. Watu hao wanajua kwamba kuabudu hiyo mifano na sanamu kumekatazwa kabisa katika Maandiko ya Biblia.
Yaendelea [Kurani Tukufu] kusema kwamba watu hao katika ibada yao kwa Mwenyezi Mungu ‘wanasujudu’, yaani, wanapiga magoti mbele zake Mwenyezi Mungu kama Daudi alivyoandika katika Zaburi (Taurati), Zaburi 95:6 “Njoni, tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za
BWANA aliyetuumba.” Katika Sura 3:114 inatuambia sisi kwamba ‘wanakataza maovu’. ‘Hao’ miongoni mwa “wao Waliopewa Kitabu” wanakataza kula vyakula najisi (haramu) kama ‘Nyama ya
nguruwe’. (Taurati) Mambo ya Walawi 11:7 “Na nguruwe, … yeye ni najisi kwenu.” Wanakataza matumizi ya vileo, tumbako, na vitu vingine vinavyodhuru (haramu) afya ya mwili ambavyo vinauangamiza. Wanaziheshimu Amri Kumi za Mwenyezi Mungu kama zilivyoandikwa
katika (Taurati) Kutoka 20. Watu hao wanasadiki kwamba tunaishi katika “Siku za Mwisho” za historia ya dunia hii…
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Tuandikie maoni yako hapa. Leave your comments here