Aya hizi ni NUKUU kutoka DivineIslam’s Qur’an Viewer software v2.913
Kurani Tukufu yasema hivi kuhusu kundi hilo la pekee, kwamba hao “ndio miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli”. Iwapo hao ni miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli, basi yale wayasadikiyo hayana budi kuwa ndiyo kweli yenyewe. Kama Mwenyezi Mungu anawaita kuwa wamo miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli, basi, sisi hatuthubutu kabisa kuwakosoa.
Lakini je! si afadhali sisi pia tungeweza kujifunza kitu kwao?
Twaona ya kwamba watu hao wa pekee wanakishikilia kile ‘Kitabu’ (Maandiko ya Biblia) ambacho
Nabii Muhammad kwa makusudi mazima alituelekeza sisi kwenye [Kitabu] hicho katika Kurani Tukufu (Al Maidah) Sura 5:46 … “Na tukawafundisha (Mitume hiyo) Isa bin Maryamu
kuyahakikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uongozi na nuru na isadikishayo yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na uongozi na mauidha kwa wamchao (Mwenyezi Mungu).”
Watu hao wanasadiki kwamba ni jukumu lao kujitoa kabisa kwa Mwenyezi Mungu pasipo kuzuia kitu, kuwa na utii kwake usio na swali. Watu hao wana maadili ya kiwango cha juu, ambayo yamejengwa juu ya Maandiko ya Biblia.