Lebo

10/06/2016

Steps to Christ

There is nothing more calculated to strengthen the intellect than the study of the Scriptures. No other book is so potent to elevate the thoughts, to give vigor to the faculties, as the broad, ennobling truths of the Bible. If God’s word were studied as it should be, men would have a breadth of mind, a nobility of character, and a stability of purpose rarely seen in these times

16/05/2016

KILE ANACHOTAKA MUNGU

Wakati huu Mungu anataka kile kile alichotaka kwa watakatifu wale wawili kule Edeni utii kamili kwa matakwa yake. Sheria yake [Amri Kumi] inaendelea kuwa ni ile ile kwa vizazi vyote. Kanuni [kipimo] kuu ya haki iliyotolewa katika Agano la Kale haijapunguzwa katika Agano Jipya. Si kazi ya Injili kupunguza nguvu ya madai ya Sheria takatifu ya Mungu [Amri Kumi] ila kuwainua wanadamu juu ili wawe mahali wanapoweza kuzishika amri zake [kumi]. Imani katika Kristo inayomwokoa mwanadamu si kama vile inavyohubiriwa na wengi. "Amini, amini," ndicho kilio chao; "mwamini tu Kristo, nawe utaokoka. Hayo ndiyo yote unayopaswa kufanya." Wakati imani ya kweli inamtegemea Kristo kabisa kwa wokovu, itamwongoza [yule aliye nayo] kwenye utii kamili kwa Sheria ya Mungu [Amri Kumi]. Imani inadhihirishwa kwa matendo.
Tena, yule mtume Yohana anatangaza, akisema, "Yeye asemaye, Nimemjua [Nimeokoka], wala hazishiki amri zake [kumi], ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake" (1 Yohana 2:4). Si salama kutegemea hisia [kujisikia moyoni] au misisimko; mambo hayo ni viongozi wasioweza kutegemewa. Sheria ya Mungu [Amri Kumi] ndiyo kanuni ya utakatifu peke yake.
 Ni kwa njia ya Sheria hiyo [Amri Kumi] tabia ya mtu itapimwa. Kama mtu ye yote anayeulizia wokovu angeuliza swali hili, "Nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?" waalimu wa siku hizi wanaofundisha utakaso wangejibu hivi, "Amini tu kwamba Yesu anakuokoa." Lakini Yesu alipoulizwa swali hilo alimwambia, "Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? Yule aliyeuliza swali hilo akamjibu, akisema, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,... na jirani yako kama nafsi yako," Yesu akamwambia, "Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi" (Luka 10:25-29).Utakaso wa kweli utashuhudiwa kwa heshima ile anayoionyesha mtu kwa bidii na kwa uaminifu wake kwa amri zote [kumi] za Mungu, kwa uangalifu wake katika kuikuza kila talanta aliyopewa, kwa maongezi yake yenye busara, na kwa kuonyesha katika kila tendo analotenda upole ule wa Kristo.

12/12/2015

KUUNGAMA DHAMBI__4

Dhambi inapozifisha hisia za kiroho, mwenye dhambi hatambui kasoro alizo nazo katika tabia yake, wala hatambui ukubwa wa dhambi aliyoitenda; na kama hajisalimishi chini ya uwezo umhakikishiao dhambi wa Roho Mtakatifu, anabaki katika hali ya kuwa nusu kipofu kwa dhambi yake. Maungamo yake si ya kweli wala hayatolewi kwa dhati.

Kwa kila kosa analoungama anaongeza kutoa udhuru kwa ajili ya njia yake mbaya huku akijipongeza, akisema kwamba laiti mambo yasingalikuwa vile, asingekuwa amefanya kosa hili au lile, ambalo kwalo anakaripiwa.

Adamu na Hawa walipokwisha kula matunda yaliyokatazwa, walijaa haya na hofu kuu. Kwanza kabisa, walifikiri namna ya kujitetea kwa ajili ya kosa lao, ili waepukane na hukumu ya kifo waliyoiogopa sana. Bwana alipowauliza habari ya kosa lao, Adamu alijibu, huku kwa sehemu fulani akiliweka kosa lile juu ya Mungu na kwa sehemu juu ya mwenzi wake: “Mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.” Yule mwanamke akamtupia lawama nyoka, akasema, “Nyoka alinidanganya, nikala.” Mwanzo 3:12,13. Kwa nini ulimwumba nyoka? Kwanini ulimruhusu aje katika Edeni? Haya ndiyo maswali yaliyojificha katika udhuru aliotoa kwa ajili ya dhambi yake, kwa njia hiyo akimshitaki Mungu kuwa anawajibika kwa anguko lao.

Roho ya kujihesabia haki mtu mwenyewe mwanzo wake ilitoka kwa yule baba wa uongo, nayo imedhihirishwa na wana na binti wote wa Adamu. Maungamo ya jinsi hii hayavuviwi na Roho wa Mungu, wala hayatakubaliwa na Mungu. Ungamo la kweli litamfanya mtu abebe dhambi yake mwenyewe, na kuiungama bila ya kuwa na udanganyifu au unafiki. Kama yule mtoza ushuru maskini, pasipo kuinua sana macho yake kuelekea mbinguni, atalia, akisema, “Mungu uniwie radhi mimi mwenye dhambi;” na wale wanaokiri dhambi zao watahesabiwa haki; kwa maana Yesu atawaombea akidai damu yake iliyomwagika kwa ajili ya mwenye dhambi atubuye.

07/12/2015

KUUNGAMA DHAMBI__3

Zamani wakati wa Samweli, Waisraeli walimwasi Mungu. Walikuwa wakiteseka kama matokeo ya dhambi zao; maana walikuwa wamepoteza imani yao kwa Mungu, walikuwa wamepoteza utambuzi wao kuhusu nguvu na hekima yake katika kulitawala taifa lile, walipoteza imani yao kuhusu uwezo wake wa kuwalinda na kuithibitisha kazi yake.

Wakampa kisogo Mfalme Mkuu wa Malimwengu, na kutamani kutawaliwa kama mataifa yale yaliyowazunguka. Kabla hawajaipata amani, walitoa ungamo hili halisi: “Tumeongeza dhambi zetu kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme.” 1 Sam. 12:19. Kosa lile lile hasa ambalo walitiwa hatiani lilipaswa kuungamwa. Kutokuwa na shukrani kwao kuliitesa mioyo yao, na kuwatenga mbali na Mungu.

Ungamo halitakubaliwa na Mungu bila ya kuwapo toba ya kweli na badiliko la maisha. Lazima badiliko dhahiri lionekane katika maisha ya mtu; kila kitu kimchukizacho Mungu ni lazima kiondolewe na kutupwa mbali. Hayo yatakuwa ndiyo matokeo ya huzuni ya kweli kwa ajili ya dhambi. Kazi ile tupaswayo kufanya kwa upande wetu imewekwa wazi mbele yetu: “Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema;takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.”

 Isa. 1:16,17. “Kama mtu mwovu akirudisha rehani, na kumrudishia mtu mali yake aliyomnyang’anya, akizifuata sheria za uzima, asitende uovu wo wote; hakika ataishi, hatakufa.” Eze. 33:15. Paulo, akiongea juu ya kazi ya toba, asema hivi: “Maana angalieni, kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii kama nini ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi! Kwa kila njia mmejionyesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.” 2 Kor. 7:11.

05/12/2015

KUUNGAMA DHAMBI__2

Wale ambao hawajajinyenyekeza mioyo yao mbele za Mungu na kuziungama dhambi zao, bado hawajalitimiza sharti la kwanza la kukubaliwa na Mungu. Kama hatujasikia toba lisilo na majuto (2 Kor. 7:10), wala hatujaziungama dhambi zetu kwa moyo wa unyenyekevu na uliovunjika, na kuyachukia maovu yetu, tutakuwa kweli hatujawahi kamwe kutafuta msamaha wa dhambi zetu; na kama hatujautafuta, basi hatujawahi kamwe kuipata amani ya Mungu. Sababu ya pekee kwa nini hatupati msamaha wa dhambi zetu zilizopita ni kwamba hatuko tayari kuinyenyekeza mioyo yetu
na kutimiza masharti ya neno la kweli.

Maagizo dhahiri yametolewa kuhusu suala hili. Ungamo la dhambi, liwe hadharani au faraghani, ni lazima litoke moyoni hasa, na litolewe kwa hiari. Mwenye dhambi asilazimishwe kutoa ungamo hilo. Wala halipaswi kutolewa kwa mzaha-mzaha tu au bila kujali, au kwa kuwalazimisha wale ambao hawana hisia yo yote juu ya hali mbaya mno ya kuchukiza ya dhambi.Ungamo lile litokalo moyoni hasa humfikia Mungu mwenye huruma isiyo na kikomo. Mtunga Zaburi asema,Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka roho huwaokoa.” Zaburi 34:18.

Ungamo la kweli daima ni la aina yake, nalo linakiri dhambi halisi zilizofanywa. Pengine ni dhambi ambazo imetupasa sisi kuzikiri kwa siri mbele za Mungu tu; pengine ni tendo baya ambalo linapaswa kuungamwa kwa mtu mmoja tu, yaani, yule aliyeathirika kutokana na tendo lile; au pengine ni kosa lililotendwa mbele ya watu lililowaumiza mioyo yao, ambalo linapaswa kuungamwa mbele yao. Lakini maungamo yote ni lazima yawe dhahiri na yakiri kosa lile lile hasa ulilolitenda.

26/08/2015

KUUNGAMA DHAMBI__1

AFICHAYE dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.” Mithali 28:13.

Masharti yanayompasa mtu kufanya ili apate rehema ya Mungu si magumu, ni ya
haki na ya maana. Bwana hataki tufanye jambo fulani zito ili tupate kusamehewa dhambi
zetu. Hatuna haja ya kufanya hija ndefu na za kuchosha kwenda mahali patakatifu, wala
kujipiga-piga kuonyesha toba yetu, ili Mungu wa mbinguni apendezwe nasi, ama kufanya
malipo kwa ajili ya makosa yetu; lakini yeye aziungamaye dhambi zake na kuziacha,
ndiye atakayesamehewa.

Mtume Yakobo asema, “Ungameni dhambi zenu (kigiriki, makosa yenu) ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa.” Yak. 5:16. Ungama dhambi zako kwa Mungu ambaye ndiye peke yake awezaye kuzisamehe, na makosa yako uliyowatendea wengine uyaungame mbele yao. Endapo umemfanyia rafiki au jirani yako kosa lililomchukiza, unapaswa kuliungama kosa lako kwake, naye ni wajibu wake kukusamehe kabisa.


Kisha yakupasa kuomba msamaha kwa Mungu, kwa sababu huyo mwenzako ni kiumbe cha Mungu, na kumfanyia mwanadamu makosa ni kumfanyia makosa Muumba na Mwokozi wake. Jambo hilo linawekwa mbele ya Mpatanishi pekee wa kweli, Kuhani wetu Mkuu, ambaye “alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi,” na ambaye aweza “kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu,” na awezaye kutusafisha uchafu wote wa dhambi. Ebr. 4:15.

17/08/2015

Waliopewa Kitabu - 3

Aya hizi ni NUKUU  kutoka DivineIslam’s Qur’an Viewer software v2.913

 

 Nukuu ili ishia hapa )

Watu hao wanasadiki kwamba ni jukumu lao kujitoa kabisa kwa Mwenyezi Mungu pasipo kuzuia kitu, kuwa na utii kwake usio na swali. Watu hao wana maadili ya kiwango cha juu, ambayo yamejengwa juu ya Maandiko ya Biblia.

 

ENDELEA HAPA 

Wanamheshimu Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mkuu kuliko wote, tena hawana mshirika ye yote (kama vile Maryamu au wale wengine waitwao watakatifu wanaoabudiwa) ambaye wanamfungamanisha na huyo Mungu kama Wakristo wengi sana wafanyavyo. Katika Injili maneno haya hunenwa: Yakobo 2:19 “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema  na katika Marko (Isa al-Masih) Kristo Mwenyewe alisema… “Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja”. Watu hao hawazisujudu sanamu katika ibada yao kama wafanyavyo Wakristo wengi sana.

Wanasadiki kwamba kuabudu sanamu au mifano iwayo yote kumekatazwa kabisa na Mwenyezi Mungu, kama ilivyoandikwa katika Taurati, Kutoka 20:4-5 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala
mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia”. Watu hao wanajua kwamba kuabudu hiyo mifano na sanamu kumekatazwa kabisa katika Maandiko ya Biblia.


Yaendelea [Kurani Tukufu] kusema kwamba watu hao katika ibada yao kwa Mwenyezi Mungu ‘wanasujudu’, yaani, wanapiga magoti mbele zake Mwenyezi Mungu kama Daudi alivyoandika katika Zaburi (Taurati), Zaburi 95:6 “Njoni, tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za
BWANA aliyetuumba.” Katika Sura 3:114 inatuambia sisi kwamba ‘wanakataza maovu’. ‘Hao’ miongoni mwa “wao Waliopewa Kitabu” wanakataza kula vyakula najisi (haramu) kama ‘Nyama ya
nguruwe’. (Taurati) Mambo ya Walawi 11:7 “Na nguruwe, … yeye ni najisi kwenu.” Wanakataza matumizi ya vileo, tumbako, na vitu vingine vinavyodhuru (haramu) afya ya mwili ambavyo vinauangamiza. Wanaziheshimu Amri Kumi za Mwenyezi Mungu kama zilivyoandikwa
katika (Taurati) Kutoka 20. Watu hao wanasadiki kwamba tunaishi katika “Siku za Mwisho” za historia ya dunia hii…